Ili kuhudumia jamii kubwa zaidi ya wafasiri, ProZ.com inatoa mtandao wa kina wa huduma za msingi, nyenzo na uzoefu ambavyo huboresha maisha ya wanachama wake. Hii hapa ni orodha na muhtasari wa vipengele vya msingi zaidi.
Mtandao wa KudoZ hutoa mfumo wa kazi wa wafasiri na wengineo ili kusaidiana kati yao na tafsiri au maelezo ya istilahi na misemo mifupi. Hadi leo, tayari kuna maswali 3,904,884 ya tafsiri yameshaulizwa. Maswali yote haya na tafsri zake zilizopendekezwa vimezalisha hifadhi muhimu yenye kutafutika.
ProZ.com ndio chanzo nambari moja cha wateja wapya kwa wafasiri. Kazi za tafsiri na ukalimani hutangazwa kupitia mfumo wa kazi, na watu waliovutiwa wanaweza kutuma makadirio ya bei. Zaidi ya mfumo wa kutangaza kazi, pia kuna saraka yenye kutafutika ya wafasiri huru na wakalimani ambayo inaweza kutumika kuwapata wataalamu wa lugha
Kuna mikutano ya ProZ.com, vikao vya mafunzo (mtandaoni na nje ya mtandao) na powwows (mikusanyiko isiyokuwa rasmi ya vikundi vya watumiaji wa ProZ.com wanaoishi katika ujirani wa karibu) vinatokea duniani kote. Hafla hizi ni njia bora ya kupanua ustadi wako, kukutana na wataalamu wapya, na kuburudika!
Bodi ya Bluu ni hifadhidata yenye kutafutika ya wasambazaji wa kazi za lugha na maoni kutoka kwa watoa huduma. Watumiaji wa ProZ.com ambao wamefanyakazi na msambazaji maalum wanaruhusiwa kuingiza nambari kuanzia 1 hadi 5 kulingana na "uwezekano wake wa kufanyakazi tena” na msambazaji aliyetolewa, pamoja na maoni mafupi. Kutokana na zaidi ya wasambazaji 15,000 kwenye faili, ni jambo la busara kukagua Bodi ya Bluu kabla ya kukubali kazi kutoka kwa mteja mpya.
Jadili kuhusu matatizo yanayohusika na kuwa mfasiri au mkalimani katika vikao kama vile Ujanibishaji, msaada wa kiufundi wa zana za kufasiria CAT, Kujikamilisha, Utapta wa filamu, n.k.