ProZ.com translation contests » Rules

1. Maingizo lazima yawe kazi asilia. Utumiaji tena au urejeleaji wa yaliyomo (mifano iliochapishwa) tafsiri, nzima au baadhi, imeharamishwa na inasababisha kufelishwa. Inawezekana kufanya na mtu mwingine, lakini lazima mtu huyo ahusishwe kama mwenza ingizo linapowasilishwa.
2. Utambulisho wa wagombezi sharti usijulikane ugombeaji unapoendelea. Wagombezi wasijadili maingizo yao, au maamuzi waliofanya kwenye mchakato wa tafsiri, kukiwa ugombeaji au upigaji kura wa ugombeaji unaendelea. Kutoa taarifa ambayo itamwezesha mwenza kubaini ni ingizo lipi lako binafsi ni kigezo cha kufelishwa.
3. Ukisiaji kwenye maingizo hahurusiwi. Ni kinyume cha sheria kukisia kuwa ni nani amewasilisha ingizo fulani.
4. Michango ya hadhara kuhusu maingizo wakati wa ugombeaji hairuhusiwi. Michango ya hadhara kuhusu maingizo (au njia wezekana kutafsiri chanzo cha matini) hairuhusiwa na mtumiaji yeyote wa Proz.com wakati wa ugombezi au nyakati za upigaji kura wa ugombeaji. Michango iliotolewa kwenye midahalo haitatathminiwa, na kama itawekwa hadharani, yatatolewa. Mjadala wa moja kwa moja wa mtu-hadi-mtu (ynk. Kwa baruapepe, n.k.) wa aina hii miongoni mwa wapiga kura inaharamishwa pia.
5. Kuhimiza wapigaji kura kupiga kwa njia fulani ni kinyume cha sharia. Kuhimiza wapigaji kura kupiga kwa njia fulani, au kuchagua ingizo Fulani, hakuruhusiwi. Kujaribu kushawishi matokeo kwa kuteua kikundi fulani cha watumiaji (kwa mfano watumiaji kutoka nchi moja) ili kupiga kura pia imeharamishwa.
6. Uhalali wa ushindi usiuliziwe hadharani. Kama maonefu yameshukiwa yaripotiwe kwa wahudumu wa wavuti kupitia kwa support request.