Kanuni za tovuti

Sheria za Utumiaji wa ProZ.com

Sheria zifuatazo zimeundwa ili kueneza na kuimarisha uzuri, anga bora ya matokeo, katika eneo la tafsiri la ProZ.com. Kwa kutumia tovuti, unaashiria ukubalifu wako, na kukubali kuzingatia sheria hizi.


Sheria ya Tovuti

1 Midahalo ya Proz.com imetolewa mahususi kwa majadiliano katika mamlaka ya Proz.com.
Mada halali ya mjadala ni lugha na huduma za lugha (tafsiri, ukalimani, ujanibishaji, upachikaji wa vijimada, n.k.), pia na biashara na masuala ya kiteknikali yaliyo ya lengo la hasa wataalamu wa lugha kwenye kazi zao. Mawasilisho yasiyohusiana na lugha au tafsiri, au biashara za lugha, au tafsiri, hayaruhusiwi. Mawasilisho yaliyo ya siasa, dini, au yaliyo pingamizi kimtazamo, au yatakayofikirika kuwa kiukaji na watumiaji wengine, yataondolewa bila kuzingatia mitazamo iliyotolewa. [Kwa maelezo, angalia wavuti Fasili ya Mamlaka ]
2 Wawekaji wanahitajika kuandika vichwa kamili na kuwekwa kwenye mdahalo unaofaa.
Kwa sababu midahalo ya Proz.com ni amilifu, umakini unahitajika ili kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali. Vichwa vya uwekaji lazima yawe bainifu kwenye uwasilisho na yaliyomo vizuri iwezekanavyo, wakati wowote uwezekanao, ili kudhihirisha lengo kuu kwenye kichwa. (Kumbuka kwamba kwa kusudi uelewa na mpangilio wa makavazi, wasimamizi wamepewa mamlaka ya kuhariri vichwa vya mawasilisho na kuhamisha mada katika midahalo. Wasimamizi hawawezi kubadilisha maudhui kwenye uwekaji wa mdahalo.)
3 Uwekaji usifanywe zaidi ya mara moja.
Usiweke mada sawa mara nyingi au kwenye midahalo mingi.
4 Majibu hafai kupotoka kutoka katika mada yaliyowekwa.
Unapojibu mada, zingatia mada ilivyowekwa. Kubadilisha mjadala ni lazima kuweka mada mpya.
5 Utani kwenye mitazamo ya wengine haukubaliwi.
Kutoa maoni kwenye mitazamo ya wengine bila idhini (‘Jenny anavyotafakari…’), hakurusiwi.
6 Wakati mada yamefungwa, mazungumzo hayataendelezwa.
Mijadala iliyo kwenye misururu iliyofungwa au iliyofichwa na wahudumu wa Proz.com au wasimamizi isiendelezwe. Uwekaji uliofanywa kwenye misururu hiyo hauwezi kuhaririwa baada ya mada kufungwa.
7 Lugha idhinishwa ya mdahalo lazima itumike.
Lugha tumizi itafafanuliwa kwa kila mdahalo, na lugha hiyo itumiwe kwa njia inayohitajika wakati wa kuweka. Mahali ambapo imeelezwa vinginevyo, Kiingereza ndio lugha ya kazi.
8 Watoaji wanaweza wasijadiliwe mahususi.
Uwekaji ama maoni kuhusiana na mtoaji kazi fulani (anayetambulika kwa jina, marejeleo, kiungo, au namna nyinginezo), iwe chanya au hasi, hayarusiwi. (Kuonyesha uwezekano wao wa kufanya tena na mtoaji kazi fulani watumiaji wa toviuti wanahitaji kutumia Proz.com Blue Board.)
9 Ni wajibu wa mwekaji kuheshimu hatimiliki.
Utumiaji wa nakala zisizoidhinishwa (hatimilikiwa, zizo na nembo ya biashara, ama iliolindwa) hairuhusiwi. Ni dondoo na viungo kwenye makala ambavyo vitachapishwa, iwapo tu umepata idhini kutoka kwa wachapishaji. Kwa visa kama hivyo, uwekaji lazima uwekwe wazi kuwa idhini imetolewa.
10 Hamna ukalimani wa sheria.
Ukalimani wa kisheria na changamoto za sheria kwenye sera na vipengele vya Proz.com havihitajiki kujadiliwa kwenye midahalo, bali vitumwe kwa maandishi kwenye makao makuu ya Proz.com.
11 Tumia sehemu tengwa ya tovuti.
Midahalo isitumiwe kwa maswala ambayo yana sehemu teule kwenye wavuti. [Unaweza ukapata orodha ya sehemu teule za wavuti hapa]
12 Uchunguzi wa mchakato wa mwungano wa WAT Idhinishwa husijadiliwe kwenye midahalo.
Kuimarisha maadili ya mchakato wa uchunguzi kwa mwungano wa WAT Idhinishwa, udhahiri wa mchakato usijadiliwe kwenye midahalo. Maelezo kuhusu tajiriba nafsi katika mchakato wa uchunguzi wa mwungano wa WAT Idhinishwa, pamoja na sababu pokelewa kwa kukubaliwa au kukataliwa kwa maombi yako, yasijadiliwe kwenye midahalo. Maswali yawasilishwe kupitia support request.
13 Kutangaza matukio yaso-ya-Proz.com kupitia midahalo kunaruhusiwa tu katika mdahalo wa “Tasnia ya Matukio Lugha & Matangazo”.
Tangazo moja linaweza wekwa kwa kila tukio katika mdahalo wa Tasnia ya Matukio Lugha & Matangazo. Matangazo zaidi (k.m “kikumbusho”,”mwito wa mwisho”) hayaruhusiwi. Matukio yasitangazwe popote pale katika midahalo. Upekee unaruhusiwa kwa aso-Mwingereza au mdahalo wa nchi-dhahiri; tukio linaweza wekwa mara moja, kwa mmoja aso-Mwingereza au mdahalo wa nchi-dhahiri (si ziada ya, lakini kwa niaba ya uwekaji katika mdahalo wa Matukio na Matangazo).

Uzingatiaji wa sheria hapo juu ni sharti la kuendelea na haki ya ufikivu na utumiaji wa tovuti.

Utekelezaji


Wafanyakazi au wasimamizi huchukua mojawapo ya hatua zifuatazo ili kutekeleza sheria zipo hapo:
* kuwasiliana na watumiaji wa tovuti ili kuhimiza uzingatifu wa sheria
* kujitoa kwenye kuidhinisha (au kutoa/kuficha) uwekaji unaokiuka sheria
*kusababisha ujumbe zinazohusiana na sheria kuonekana kwa watumiaji fulani wanapochukua hatua fulani
* kusimamisha, kwa muda au milele, ufikiaji wa vibambo ambavyo vimetumiwa kukiuka sheria.
* ukatishaji wa umbo au uanachama (wafanyakazi pekee)

Wasimamizi na wafanyakazi sharti wafanye kulingana na, na wanakingwa na, sheria za tovuti sawia na wanachama wengine.

Ukatishaji

Kwa nadra sana matukio ya ukiukaji, wafanyakazi wa ProZ.com hukatiza umbo (na uanachama) kwa athari hiyo. Mara nyingi, hata hivyo, ProZ.com hutumia sera ya “kadi manjano/nyekundu” ulingano wa kadi manjano/nyekundu kwenye kandanda/soka, ukatishaji.

Kadi manjano na nyekundu hutolewa tu na wafanyakazi. Sheria zinaonyeshwa kwa nambari, na tarehe ya kadi inaingizwa. Istilahi “kadi manjano” au ”kadi nyekundu” zinatumika wazi; kama baruapepe imetumwa, istilahi uonekana katika kifungu mada.

Mtumiaji wa tovuti ambaye amepewa kadi ya manjano anaweza kuendelea kutumia tovuti (wakati mwingine kwa vikwazo fulani), lakini hata hivyo kuna arifa kwamba ukiukaji zaidi utasababisha ukatishaji. Mtu ambaye umbo lake limekatizwa hakubaliwi tena katika ProZ.com.

Watoajikazi wanawajibikia sera ya ukatishaji.

Ufafanuzi

Kwa ufafanuzi wa sheria hizi au utekezaji wa sheria, tafadhali wasilisha ombi la msaada.

Request help


Site Documentation


The member services and support team
Jared

Jared

Lucia

Lucia

Helen

Helen

Yana

Yana

Karen

Karen

Evelio

Evelio

Hayjor Roca

Hayjor Roca

Andrea

Andrea

Naiara Solano

Naiara Solano

Joseph Oyange

Joseph Oyange

Isabella Capuselli

Isabella Capuselli

Saint Machiste

Saint Machiste

Valentin Zaninelli

Valentin Zaninelli

Laura Rucci

Laura Rucci

Erika Melchor

Erika Melchor

Charlotte Gathoni

Charlotte Gathoni

Agostina Menghini

Agostina Menghini

Tanya Quintery

Tanya Quintery

Benedict Ouma

Benedict Ouma

All of ProZ.com
  • All of ProZ.com
  • Kutafuta neno
  • Kazi
  • Mabaraza
  • Multiple search