Kanuni za tovuti
Sheria za Utumiaji wa ProZ.com
Sheria zifuatazo zimeundwa ili kueneza na kuimarisha uzuri, anga bora ya matokeo, katika eneo la tafsiri la ProZ.com. Kwa kutumia tovuti, unaashiria ukubalifu wako, na kukubali kuzingatia sheria hizi.
Kategoria
Sheria ya Tovuti
1.1 |
“Msaada” na faharasa-jengwa ya Kudoz yanatolewa tu kwa istilahi msaada na ujengaji wa faharasa mtawalia.
Utumizi wa mfumo kwa kujitangaza, mijadala, au lengo mbali na kupata au kutoa msaada kwa istilahi ni haramu. |
1.2 |
Kudoz imefungamanishwa kwenye mamlaka ya lugha tu.
Uwekaji wote unaohusiana na Kudoz sharti ujifungishe katika mamlaka ya mada ya istilahi. Michango ya binafsi, katika Kudoz kama kwingineko, imeharamishwa kabisa. |
1.3 |
Makabrasha ya matini yanaweza kutumiwa tu kwa lengo nuiwa.
Kwa mfano:
Utumizi wa fomu za nyuga hapo juu kwa lengo kinyume na lililoelezwa ni haramu. Kwa mfano mchango kama ‘Nilisomea matibabu kwa miaka 3’ sharti iingizwe kwenye kabrasha la ufafanuzi, si kwenye makabrasha ya marejeleo. |
1.4 |
Fomu ya faharasa sharti itunzwe.
Faharasa za rasimu zinaundwa kiotomatiki kutoka maswali na majibu ya Kudoz. Kwa sababu, usemi kama “angalia hapo chini”, “kwa muktadha huu”, n.k., isiingizwe kwenye makabrasha ya istilahi, unapoweka chanzo cha istilahi au kupendekeza tafsiri. Kiulizi, alama ya nukuu, herufi kubwa zisizohitajika na chochote kile ambacho hakitapatikana kwenye kamusi, kiziingizwe. Tafsiri zilizoingizwa kwa ujengaji-faharasa wa Kudoz sharti ijumuishe istilahi tafsiriwa, ufafanuzi na angalau mfano tumizi, yote kwa lugha lengwa husika. |
1.5 |
Umakini unapaswa kuzingatiwa ili kutoweka wazi taarifa siri katika uwekaji wa Kudoz.
Kwa mara nyingi, majina ya wateja hayafai kuwekwa wazi kwenye uwekaji wa Kudoz. Uzingatiaji uwepo kama istilahi au muktadha utaweka wazi taarifa siri kwa mazingira yake. |
Uzingatiaji wa sheria hapo juu ni sharti la kuendelea na haki ya ufikivu na utumiaji wa tovuti.
UtekelezajiWafanyakazi au wasimamizi huchukua mojawapo ya hatua zifuatazo ili kutekeleza sheria zipo hapo:
* kuwasiliana na watumiaji wa tovuti ili kuhimiza uzingatifu wa sheria
* kujitoa kwenye kuidhinisha (au kutoa/kuficha) uwekaji unaokiuka sheria
*kusababisha ujumbe zinazohusiana na sheria kuonekana kwa watumiaji fulani wanapochukua hatua fulani
* kusimamisha, kwa muda au milele, ufikiaji wa vibambo ambavyo vimetumiwa kukiuka sheria.
* ukatishaji wa umbo au uanachama (wafanyakazi pekee)
Wasimamizi na wafanyakazi sharti wafanye kulingana na, na wanakingwa na, sheria za tovuti sawia na wanachama wengine.
Ukatishaji
Kwa nadra sana matukio ya ukiukaji, wafanyakazi wa ProZ.com hukatiza umbo (na uanachama) kwa athari hiyo. Mara nyingi, hata hivyo, ProZ.com hutumia sera ya “kadi manjano/nyekundu” ulingano wa kadi manjano/nyekundu kwenye kandanda/soka, ukatishaji.
Kadi manjano na nyekundu hutolewa tu na wafanyakazi. Sheria zinaonyeshwa kwa nambari, na tarehe ya kadi inaingizwa. Istilahi “kadi manjano” au ”kadi nyekundu” zinatumika wazi; kama baruapepe imetumwa, istilahi uonekana katika kifungu mada.
Mtumiaji wa tovuti ambaye amepewa kadi ya manjano anaweza kuendelea kutumia tovuti (wakati mwingine kwa vikwazo fulani), lakini hata hivyo kuna arifa kwamba ukiukaji zaidi utasababisha ukatishaji. Mtu ambaye umbo lake limekatizwa hakubaliwi tena katika ProZ.com.
Watoajikazi wanawajibikia sera ya ukatishaji.
Ufafanuzi
Kwa ufafanuzi wa sheria hizi au utekezaji wa sheria, tafadhali wasilisha ombi la msaada.